Swahili quotes
Sunday, June 29, 2014
STOLEN DESTINY PART 1
“When all people you love and care, turn against your inner voice. They push you to hell, and your destiny is stolen. Now you are back with no love, no life in you, but desire to turn the world upside down”
STOLEN DESTINY PART 1
Life is a journey; and the roads we travel have twisted turns; which sometime lead us to unexpected places, and to unexpected people. I met this guy; who then with only one night he destroyed my life forever. It’s the night that my stress pushed me into hell. The night with no stars, no hope and no life in me.
Saturday, June 28, 2014
THE FAKE PRESIDENT/Rais Feki sehemu ya 1
Mtu yeyote anaweza kukua, kujifunza na kuwa Rais. Lakini, si kila Rais anaweza kufanya, kusababisha mabadiliko na mapinduzi makubwa kiuchumi,kijamii na kisiasa. Kiti cha Urais; ni kwaajili ya mtu maalumu mwenye tabia iliyotukuka na mtu wa watu, tabia kubwa,mgumu, mwenye uwezo mkubwa kiakili, maono makubwa, msimamo mkali,mzalendo na mwenye njaa ya mabadiliko asiyeendeshwa na watu wala matukio. Ni kwa mara ya kwanza Tanzania inampata Rais mwenye uwezo mkubwa uliotukuka. Mwenye maono makubwa . Mwenye hekima. Mwenye upendo wa dhati. Mzalendo wa kweli. Jasiri. Mtu wa watu. Mh. Kennedy P. Kyando; rais mpya aliyeshinda kwa kishindo kupitia chama cha upinzani kiichwacho people's welfare party(pWp).
Friday, June 27, 2014
MAISHA YANGU DUNIANI SEHEMU YA PILI
MAISHA YANGU DUNIANI.
"Mahojiano kati ya Mimi na Mungu"
Simulizi ya uamsho.
Kabla sijaondoka duniani niliishi maisha ya bora liende. Nilitumika na watu wenye ndoto kubwa kama spea ya trekta. Dini yangu, nilijivunia dini yangu na kupumbazika kwa majivuno. Wale waliotofautiana na mimi; niliwatenga na kuwahukumu kama Mungu. Sikujua ukweli. Sikujua kuwa yote niliyosoma. Yote yaliyokuwa kichwani mwangu yalikuwa ni upupu tu. Yaliniendesha na kunifanya niishi kama mashine isiyo na roho kwa ndani. Nilijikuta miaka yangu inakimbia tu; hakuna cha maana nilichofanya duniani.
Thursday, June 26, 2014
SIRI INAYOANGAMIZA SEHEMU YA PILI.
SIRI INAYOANGAMIZA SEHEMU YA PILI.
"Beee mama" Helena aliitika na kumwacha Steve bado ameduwaaa chumbani kwake. Alipofika sebuleni alikuta mama yake amesimama, mkono wake wa kulia umeshikilia kitambaa cha kusafishia vyombo.
"Steve anafanya nini chumbani kwako?" Mama aliuliza.
"aah! alikuwa anauliza kama kuna rafiki yangu yeyote alikuja jana"
Wednesday, June 25, 2014
NAIJUTIA NDOA YANGU...SEHEMU YA KWANZA
Ilikuwa kama ndoto kuolewa na mtoto wa waziri mkuu. Benson Mkama. Siku ya harusi ilikuwa ni balaa. Nilikuwa na furaha isiyo kifani. Nilijua kuwa umaskini sasa basi. Padri akasema
"Benson Mkama, unamkubali Jackline Stephano kuwa mke wako, katika shida na raha; katika hali zote mpaka kifo kitakapowatenganisha?"
Niliolewa na kaka yangu sehemu ya 2
NILIOLEWA NA KAKA YANGU SEHEMU YA PILI.....
'Mungu chukua uhai wangu..chukua uhai wangu nimechoka kuishi mateso ya dunia'
Baba alimsogelea mama huku mkono wake wa kulia umeshika mkanda wa suruali yake. Mama akiwa uchi wa mnyama, amejikunja chini kwa uoga kama kifaranga. Mama Hamis naye amekaba shingo yangu; kunizuia nisiokoe maisha ya mama yangu. Mdogo wangu Shadrack yupo pembeni ya mama analia kama yatima. Bila huruma, bila kujali baba aliinua mkono wake wenye mkanda na kuanza kumsulubu mama mbele ya macho yetu. Mbele ya hawala yake.
Tuesday, June 24, 2014
Nikumbuke Mpenzi wangu part 2
Mungu nimekosa nini. Mungu nisaidie.....Nikasikia sauti ya madaktari wakipumua kwa furaha. Michael akasema; "Dokta...umemrudisha". Wote kwa pamoja wakafurahi. Dokta Adam alionyesha kufurahi zaidi. Sauti yake ya furaha; ilipenya ndani ya masikio yangu. Hii ilinipa amani; nikajua labda nimerudi. Wote wakavua glovu na kuzitupia ndani ya chombo cha kuutupia uchafu. Niliwasikia kwa makini sana, nilitaka kujua ni kitu gani kinaendelea. Baada ya dakika kadhaa nikasikia sauti ya Debora.
Friday, June 20, 2014
MAISHA YANGU DUNIANI PART 1: MAHOJIANO KATI YA MUNGU NA MWANADAMU
MAISHA YANGU DUNIANI PART 1: KILA IJUMAA.
Ilikuwa tarehe 12/06/1982, siku nilipokufa na kuondoka duniani. Ni siku niliyokutana na Mungu uso kwa uso, katika ulimwengu mwingine, unaofahamika kwa majina mengi; wengine huita mbinguni, wengine Ahera, kulingana na imani tofauti. Nikiwa nimebeba mizigo yangu ya ndoto nilizoshindwa kuzifikia duniani, mawazo niliyoogopa kuyatoa, vipaji na zawadi nilizopewa na Mungu nivitumie;
Nilipofika geti la mbinguni; nilikutana na malaika. Nilisalimia; kwa heshima. Na kujibiwa;
"Hiyo mizigo ya ndoto zako,vipaji na zawadi za maisha hairuhusiwi kuingia nayo mbinguni. Mungu alikupa ili itumike duniani na siyo mbinguni. Kwani wewe ulikuwa unafanya nini duniani miaka 89 yote iliyopita? Umekufa ukiwa na miaka 89, hujatumia hata kitu kimoja? Hapana; huwezi kuingia. Ondoka hapa"
Thursday, June 19, 2014
"Siri Inayoangamiza" :The Secret that kills: Part One...........REVISED
"Siri Inayoangamiza" Part One...........REVISED
"Maisha yako yapo salama, kwasababu huijui siri. Lakini kutokuijua siri; huyajui maisha. Na kamwe hutaujua utamu wa maisha" -SIRI INAYOANGAMIZA
Ilikuwa tarehe 31/12/2000 siku ya Jumapili muda wa saa sita na nusu usiku, Steven Mtambaji muigizaji maarufu wa filamu za kitanzania akiwa amelala katika chumba chake mbezi beach – Dar Es Salaam. Alisikia sauti ya kike ikiita "Steve…Steve...nifungulie". Alishtuka kutoka usingizini. Na kwenda kufungua mlango.
Wednesday, June 18, 2014
NILIOLEWA NA KAKA YANGU: I married my blood brother part 1.
NILIOLEWA NA KAKA YANGU: Based on a true story KILA JUMATANO.
Nikasikia sauti kutoka moyoni mwangu ikiniambia “Tulia moyo wangu. Tulia mwanangu haya yote yatapita. Haya yote yataisha. Ipo siku, ipo siku dunia yako itabadilika”.
Niliposikia sauti hiyo nilifuta machozi na kukificha kisu, ambacho kama siyo sauti hiyo ningemchoma baba yangu mzazi tumboni. Nilikaaa chini kuyasikilizia maumivu. Baba yangu hakuonyesha kujali; aliendelea kumpiga mateke mama yangu. Nilishindwa kuyavumilia, ndiyo nilishindwa kuyavumilia nilimsogelea na kumchoma mapaja yake.Kwasababu sikutumia nguvu kutokana na uoga; sikumuumiza. Alinigeukia na kunikanyaga bila huruma bila kujali kuwa mimi ni mtoto wa miaka nane. Mama akapiga kelele;
Tuesday, June 17, 2014
Nikumbuke Mpenzi wangu:Remember me my love Part 1
“Dokta Adam….Dokta Adam hatutaweza kumrudisha mgonjwa huyu. Lazima tutampoteza”
Ilikuwa ni sauti ya mwanamke niliyoisikia kwa mbali. Nilijaribu kufanya kila ninachoweza lakini mwili wangu haukuwa na uwezo tena. Sikujua nipo wapi na kwanini. Macho yangu hayakuwa na uwezo wa kuona. Pua yangu; haikuweza kuambulia harufu yoyote.
Nilianza kujiuliza kuhusu sauti ya mwanamke iliyosikika kupitia masikio yangu ikisema Dokta Adam hatutaweza kumrudisha mgonjwa huyu. Lazima tutampoteza. Nilijiuliza mgonjwa huyo ni nani? Je ni mimi au ni mtu mwingine? Na hapa nipo wapi? Nimefikaje?Wakati bado najiuliza maswali yasiyo na majibu nikasikia sauti ya kiume ikisema:“Patricia..Patricia huwezi kufia katika mikono yangu. Mateso uliyoyapata kwasasa yanatosha. Huwezi kufa. Huwezi kufia ndani ya chumba changu cha operesheni. Huwezi kufa… amka….amka Patricia”
Subscribe to:
Posts (Atom)