Swahili quotes
Sunday, June 29, 2014
STOLEN DESTINY PART 1
“When all people you love and care, turn against your inner voice. They push you to hell, and your destiny is stolen. Now you are back with no love, no life in you, but desire to turn the world upside down”
STOLEN DESTINY PART 1
Life is a journey; and the roads we travel have twisted turns; which sometime lead us to unexpected places, and to unexpected people. I met this guy; who then with only one night he destroyed my life forever. It’s the night that my stress pushed me into hell. The night with no stars, no hope and no life in me.
Saturday, June 28, 2014
THE FAKE PRESIDENT/Rais Feki sehemu ya 1
Mtu yeyote anaweza kukua, kujifunza na kuwa Rais. Lakini, si kila Rais anaweza kufanya, kusababisha mabadiliko na mapinduzi makubwa kiuchumi,kijamii na kisiasa. Kiti cha Urais; ni kwaajili ya mtu maalumu mwenye tabia iliyotukuka na mtu wa watu, tabia kubwa,mgumu, mwenye uwezo mkubwa kiakili, maono makubwa, msimamo mkali,mzalendo na mwenye njaa ya mabadiliko asiyeendeshwa na watu wala matukio. Ni kwa mara ya kwanza Tanzania inampata Rais mwenye uwezo mkubwa uliotukuka. Mwenye maono makubwa . Mwenye hekima. Mwenye upendo wa dhati. Mzalendo wa kweli. Jasiri. Mtu wa watu. Mh. Kennedy P. Kyando; rais mpya aliyeshinda kwa kishindo kupitia chama cha upinzani kiichwacho people's welfare party(pWp).
Friday, June 27, 2014
MAISHA YANGU DUNIANI SEHEMU YA PILI
MAISHA YANGU DUNIANI.
"Mahojiano kati ya Mimi na Mungu"
Simulizi ya uamsho.
Kabla sijaondoka duniani niliishi maisha ya bora liende. Nilitumika na watu wenye ndoto kubwa kama spea ya trekta. Dini yangu, nilijivunia dini yangu na kupumbazika kwa majivuno. Wale waliotofautiana na mimi; niliwatenga na kuwahukumu kama Mungu. Sikujua ukweli. Sikujua kuwa yote niliyosoma. Yote yaliyokuwa kichwani mwangu yalikuwa ni upupu tu. Yaliniendesha na kunifanya niishi kama mashine isiyo na roho kwa ndani. Nilijikuta miaka yangu inakimbia tu; hakuna cha maana nilichofanya duniani.
Thursday, June 26, 2014
SIRI INAYOANGAMIZA SEHEMU YA PILI.
SIRI INAYOANGAMIZA SEHEMU YA PILI.
"Beee mama" Helena aliitika na kumwacha Steve bado ameduwaaa chumbani kwake. Alipofika sebuleni alikuta mama yake amesimama, mkono wake wa kulia umeshikilia kitambaa cha kusafishia vyombo.
"Steve anafanya nini chumbani kwako?" Mama aliuliza.
"aah! alikuwa anauliza kama kuna rafiki yangu yeyote alikuja jana"
Wednesday, June 25, 2014
NAIJUTIA NDOA YANGU...SEHEMU YA KWANZA

Ilikuwa kama ndoto kuolewa na mtoto wa waziri mkuu. Benson Mkama. Siku ya harusi ilikuwa ni balaa. Nilikuwa na furaha isiyo kifani. Nilijua kuwa umaskini sasa basi. Padri akasema
"Benson Mkama, unamkubali Jackline Stephano kuwa mke wako, katika shida na raha; katika hali zote mpaka kifo kitakapowatenganisha?"
Niliolewa na kaka yangu sehemu ya 2
NILIOLEWA NA KAKA YANGU SEHEMU YA PILI.....
'Mungu chukua uhai wangu..chukua uhai wangu nimechoka kuishi mateso ya dunia'
Baba alimsogelea mama huku mkono wake wa kulia umeshika mkanda wa suruali yake. Mama akiwa uchi wa mnyama, amejikunja chini kwa uoga kama kifaranga. Mama Hamis naye amekaba shingo yangu; kunizuia nisiokoe maisha ya mama yangu. Mdogo wangu Shadrack yupo pembeni ya mama analia kama yatima. Bila huruma, bila kujali baba aliinua mkono wake wenye mkanda na kuanza kumsulubu mama mbele ya macho yetu. Mbele ya hawala yake.
Subscribe to:
Posts (Atom)





