Swahili quotes

Saturday, January 19, 2013

Wake Up from the prisoned mind and be yourself





A Man was once a child created through love, the child was once in the womb of a mother connected to God.  While Man is in his mother’s womb; God bestowed his blessings upon him, then he implanted within a man the power to love, the power to think, the power to create, the power to plan, the power to imagine, the power to will, the power to speak, the power to heal, , the power to pray, the power to laugh, the power to choose and the power to do the impossible and be anything for a purpose.

Friday, January 18, 2013

Jinsi ya Kuthibiti Hasira

Jinsi ya Kuthibiti  Hasira


Maisha ya mwanadamu ni  mzunguko wa changamoto mbalimbali, kila dakika ya maisha yako, kila sehemu uliyopo  na kila mahusiano  uliyonayo vyote vimebeba  changamoto na maana Fulani ya maisha yako.
Wote tunapitia maumivu,machungu, makwazo , kero na mifumo ya aina moja lakini kinachomtengeneza na kumboresha mtu si yale anayoyapitia - bali ni yale anayoyafanya kutokana na yale anayoyapitia. Katika mahusiano tunakumbana na watu,marafiki na hata wapenzi wetu  wanaotupandisha hasira na mara nyiningine wanaotutenda vibaya haswa, lakini cha muhimu kufahamu ni kuwa yote haya ni shule ili tukue na tupanuke zaidi. 

Thursday, January 17, 2013

Wewe ni upendo na kweli




Wewe ni Upendo na kweli……Kutoka katika kitabu cha Jitambue; ukurasa wa 13.
Wewe ni Upendo na kweli
Siku moja nilialikwa redioni, na nikaulizwa swali “Geophrey ni nini maana ya maisha?” nikajibu maisha ni upendo. Mtangazaji alishangaa, nilivyojibu kwa kifupi na bila nyongeza yoyote.  

Naijutia ndoa yangu



"Naijutia Ndoa Yangu; Sura Ya Kwanza; page one"
Ilikuwa kama ni ndoto, mie kuolewa na mtoto wa waziri mkuu ambaye alikuwa anaandaliwa kuwa rais kwa miaka ya baadaye. Siku ya harusi yetu ilikuwa ni balaa, kila magazeti yaliandika habari kuhusu ndoa yetu kwa stail zao.

Wednesday, January 16, 2013

JIULIZE WEWE NI NANI? JITAMBUE....




 JIULIZE WEWE NI NANI? JITAMBUE....

Mimi ni nani? Ni swali lenye msukumo wa ndani. Jina lako si wewe, jina lako haliwezi kujibu; kwasababu jina lako ni jina walilolipenda wazazi wako na wakakupa.