Swahili quotes

Thursday, January 17, 2013

Wewe ni upendo na kweli




Wewe ni Upendo na kweli……Kutoka katika kitabu cha Jitambue; ukurasa wa 13.
Wewe ni Upendo na kweli
Siku moja nilialikwa redioni, na nikaulizwa swali “Geophrey ni nini maana ya maisha?” nikajibu maisha ni upendo. Mtangazaji alishangaa, nilivyojibu kwa kifupi na bila nyongeza yoyote.  

Mwanadamu anaishi lakini hajui maana ya maisha, maana ya maisha duniani ipo katika maana ya upendo. Maisha ni upendo na upendo ni maisha. Kama hujui upendo ni nini; hujui maisha.Wanadamu, wanajua kuna kitu kinaitwa Upendo kutokana na wanavyoongea, katika vitabu, TVs,radio, mazungumzo na katika maisha ya kila siku; mfano mtu anaweza kusema; nampenda mke wangu, nampenda mume wangu, nampenda mungu, nawapenda watoto wangu, nampenda mpenzi wangu lakini hawajui nini maana halisi ya Upendo. 

NenoUpendo linatumika sana lakini ni wachache sana wanaojua maana yake. Wengine wanadhani Upendo ni kitu Fulani kinachotumika katika mahusiano,maongezi na hata maisha mengine, wakati upendo ni maisha.

Mwanadamu ni maisha, upendo ni maisha na kama upendo ni maisha basi mwanadamu ni upendo. Kuishi ni kupenda, kama hupendi wewe ni marehemu.  Maisha bila upendo hamna maana, hamna maisha. Asili ya maisha ni upendo. Sote bado tunaishi kwasababu kwa kiasi Fulani tumeunganishwa na upendo. Kila kitu duniani kimeunganishwa na upendo; mazingira, mimea,wanyama,mwanadamu na Mungu wote tumeunganishwa na upendo. Hewa unayovuta na kutoa ni ya bure, kutokana na mfumo uliumbwa na kuunganishwa na upendo. Mimea haiwezi kuishi bila sisi, kutokana na hewa tunayotoa bure kwa mfumo wa upendo, hali kadhalika sisi hatuwezi kuishi bila mimea kutokana na mfumo tunaounganishwa wa upendo.

Maswali yote uliyonayo juu ya Mungu, kwanini humuoni, kwanini hakufuatilii unaishi vipi wala; kukuamrisha ni kitu gani ufanye, shida zako, utajiri, au umaskini wako; vyote vimejificha katika maana ya upendo.

Upendo ni zaidi ya dini yako, upendo ni zaidi ya siasa na serikali yako. Chochote unachofanya nje ya upendo ni feki, ni uongo, ni kupoteza muda . Hata kiwango cha amani moyoni mwako na furaha ni kutokana na upendo. Miujiza ya maisha, kupona kwa watu, Baraka na kila aina ya mazuri duniani, ni kutokana na upendo. Upendo ni zaidi ya mali na utajiri wa aina yoyote, na zaidi upendo haununuliwi. Upendo wa kweli ni upendo unaotoa na si kupokea, kupenda ni kutoa upendo kusubiri kupendwa.

Tumefundishwa kuwa kuna dalili za mwisho wa dunia, utasikia mwisho wa dunia umekaribia hii si kweli. Dunia hii inaumwa, na inaumwa si kwasababu ya dalili za mwisho wa dunia lakini ni kwasababu ya kukosekana kwa upendo. Upendo ukipotea; ni mwisho wa dunia.

Zaidi ya akili, tunahitaji upendo; kwasababu akili inaweza kudhuru na upendo unaweza kuponya. Zaidi ya sheria tunahitaji upendo, kwasababu sheria ni kipofu na inaweza kumuonea mnyonge. Zaidi ya sala na maombi, tunahitaji upendo kwasababu sala na maombi si kitu kama hakuna upendo.

Zaidi ya dini tunahitaji upendo; kwasababu dini muda mwingine huwa chanzo cha utengano na kubaguana wakati sisi sote ni roho moja na tumetoka sehemu moja na tutarudi sehemu moja. Upendo husamehe yote, upendo hautakabali, upendo haudai malipo, upendo ni amani, upendo haulazimishi, upendo huelewa, upendo ni upole na zaidi husaidia. Kupenda ni kumuacha Yule umpendae, afanye atakavyo, achague apendavyo kwa uhuru wake ajifunze mwenyewe hata kama akifanya makosa.


Kumbuka maisha si idadi ya miaka unayoishi, bali ni idadi ya watu uliowagusa kutokana na upendo.  
 
PATA NAKALA YA KITABU HIKI KWA KUFANYA YAFUATAYO...

 1. TUMA EMAIL YAKO KWA NAMBA 0755306799.
 2.  TUMA TSHS.3000 KWA  M-PESA KWA NAMBA 0755306799,
 3.  UTATUMIWA SOFT COPY YA KITABU HIKI; KUPITIA EMAIL YAKO.

KWA MAELEZO ZAIDI PIGA SIMU;0755306799.
EMAIL:gtlivemore@gmail.com

UKITAKA VITABU VINGINE ZAIDI VYA Geophrey Tenganamba, kama;
NAIJUTIA NDOA YANGU, KICHWA CHAKO NI DHAHABU, JITAMBUE, THE RICHEST GOLDMINE IN YOU,THE LOVE OF MY LIFE,NGUVU YA KUJITAJISRISHA ILIYOKO NDANI YAKO, I MARRIED A MONSTER, THE POWER OF A WOMAN NA VINGINE VINGI TUMIA MAWASILIANO HAPO JUU.....

No comments:

Post a Comment