"Siri Inayoangamiza" Part One...........REVISED
"Maisha yako yapo salama, kwasababu huijui siri. Lakini kutokuijua siri; huyajui maisha. Na kamwe hutaujua utamu wa maisha" -SIRI INAYOANGAMIZA
Ilikuwa tarehe 31/12/2000 siku ya Jumapili muda wa saa sita na nusu usiku, Steven Mtambaji muigizaji maarufu wa filamu za kitanzania akiwa amelala katika chumba chake mbezi beach – Dar Es Salaam. Alisikia sauti ya kike ikiita "Steve…Steve...nifungulie". Alishtuka kutoka usingizini. Na kwenda kufungua mlango.
Alipofungua mlango, alishtuka kukutana na msichana mzuri asiyemfahamu. Huu ni usiku. Huyu msichana ni nani? Na anataka nini?Msichana alikuwa amevaaa nguo za kulalia kwa lugha ya kigeni huita night dress zenye rangi nyeupe. Ilimpa shida sana. Akauliza;
“wewe ni nani?"
Msichana akajibu; “Mimi ni Nas”.
Steven akauliza tena ; "Nas? Nas yupi? Na umekuja kufanya nini usiku huu? Mbona sikufahamu? "Msichana akacheka kwa upole na kujibu kwa kujiamini;
“Jamani mbona maswali mengi? Niruhusu niingie ndani kwanza".
Moyoni mwake akasikia sauti ikimwambia usimruhusu usimruhusu. Mwili wake ukatamani maumbile yake, hisia zake zikamzidi urefu, akaanza kusisimka.Kila akijitahidi kuzuia hisia zake; inashindikana. Hii kitu gani inanitokea? Alijikuta anababaika. Akiwa amesimama kama sanamu ya kiume mlangoni, msichana akasema;
"Niruhusu niingie Steve jamani. Dakika moja tu"
Hisia zake zikazidi kumpanda. Hawezi. Hajiwezi tena. Mwisho akaamua. Liwalo na liwe. Akaamua kumruhusu msichana aingie.
Msichana alipoingia chumbani kwa Steve; alitoa nguo yake ya kulalia {night dress) kwa haraka bila aibu,bila wasiwasi na bila kuombwa. Steve alibaki anashangaa kama mtu aliyeshikwa akili.Hii ni kitu gani? Huyu msichana ni nani? Ni shetani? Ni malaika? Au ni watembea usiku?
Akiwa bado yupo kwenye mshangao; yule msichana akamsogelea. Steven akarudi nyuma. Kila hatua aliyochukua kumsogelea, Steve naye alirudi nyuma kumkwepa. Ikabidi aulize;
"Wewe ni nani?"
Msichana akacheka. Na kusema "Mimi ni rafiki wa dada yako Helena".
Steve alipotaka kuuliza swali jingine. Msichana akamfuata na kumkumbatia kwa nguvu.Steve hakuwa na uwezo tena. Hisia zake zilikuwa zimepata ushindi.
Akajikuta hajiwezi, hajitambui na akabaki analalamika wewe ni nani...wewe ni nani...wewe ni nani....Bila kujua anafanya kosa kubwa la maisha yake. Akambeba kama mke wake na kumpeleka mpaka kitandani. Alimbeba kwa nguvu na kumpeleka mpaka kitandani. Moyo wake ulikuwa mzito, lakini hisia zake zilikuwa kali. Walilala pamoja. Ilipofika saa tisa; Steve amechoka taabani.
Hiyo ilikuwa mara yake ya kwanza katika maisha yake kukutana na msichana wa aina hiyo. Mwenye uwezo wa kipekee na ujanja usiopimika. Kutokana na raha aliyopewa; hakutaka kuhoji zaidi. Akajiachia na kuituliza sauti ya moyoni; iliyokuwa inamzuia asifanye kosa hilo. Wasiwasi hakuna tena. Hakujua ameingia mkataba na dunia nyingine. Mkataba ambao gharama yake; ni damu. Mkataba utakaopoteza watu muhimu wa maisha yake. Huku akitabasamu akauliza;"Haya sasa. Niambie wewe ni nani?"Msichana akacheka. Wote wakacheka. Steve akauliza tena ; "Wewe ni nani?"Msichana akajibu "kesho asubuhi muulize Helena. Jibu utakalolipata; litakupa picha mimi ni nani"Steve hakuridhika na majibu hayo; akamkazia macho : "Nataka wewe. Nataka uniambie wewe ni nani please".Msichana akacheka. Na kumrukia juu ya kifua chake. Na kumfumba macho. Baada ya sekunde tano; Steve alipoteza fahamu. Akalala usingizi mzito, mpaka alipoamka saa kumi na mbili asubuhi baada ya kusikia mwito wa simu ya mpenzi wake Irene ; akapokea simu ;"Halo...halo""Mambo vipi Steve wangu; Umeamkaje?""Salama"."Vipi, mbona unajibu kwa uchovu sana?""Nimechoka. Bado nina usingizi"Waliongea ya kwao. Walipomaliza; Steve alishangaa sana kukuta yupo mwenyewe kitandani na amevaa saa yenye rangi ya dhahabu. Na chini ya mto wake kuna karatasi imeandikwa; nimekuachia zawadi ya saa. Asante sana. By Nas.
Zaidi Chumba chake chote, kilikuwa kinanukia malashi ya msichana huyo; akayakumbuka yote waliyoyafanya usiku ule, ingawa alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na marafiki wengi wa kike pamoja na mchumba wake Irene hakuwahi kupewa huduma ya aina hiyo katika maisha yake yote.Aliinuka na kwenda mpaka bafuni kujisafisha vizuri, kutokana na uchafu wa aliyoyafanya usiku . Akacheka, na kusema duh huyu msichana kiboko. Sijui Helena amemtoa wapi. Baada ya kujiandaa alitoka nje na kwenda sebuleni; na kukuta dada yake ameandaa chai. Walisalimiana;"Vipi Sista umeamkaje?“ Helen akajibu; "Poa, Handsome boy, za usingizi"Akajibu na kuuliza : "Ni nzuri, mwenzako Nas, yuko wapi au bado amelala?"Helena akauliza; "Nas yupi? Mbona sina rafiki yeyote anayeitwa Nas? "Steve akauliza tena huku akitabasamu, alidhani labda Helena , anafahamu kilichotendeka usiku na anajifanya hajui ili kutaka kumtania; "Helen acha utoto, au unataka nyumba zima wajue nilichofanya jana usiku na Nas, hebu niambie; jana hukumwambia Nas aje katika chumba changu?"Helen akajibu kwa msisitizo, na kwa kuonyesha kuwa kweli hafahamu habari yoyote inayohusu Nas,
"Kaka Steve, au umetoka usingizini? Sina rafiki anayeitwa Nas, na hapa nyumbani hakuna rafiki yangu yeyote aliyekuja jana"
"Ni nani huyo unayesema nilimwambia aje kwako? Siwezi kumwambia mtu aje, bila kukutambulisha, na najua nina wifi yangu ninayempenda Irene. Siwezi kufanya ujinga huo"
Steven hakuamini alichoambiwa. Akabaki mdomo wazi. Akakumbuka yote yaliyotokea usiku. Akadhani labda amekosea kutaja jina. Huyu msichana ni nani? Au ni ndoto tu za usiku?Akataka kumwambia mdogo wake; kuhusu yaliyotokea usiku. Akaogopa. Hapana italeta picha mbaya. Ni aibu mbele ya mdogo wangu. No.Steven kauliza tena; "Helena, una uhakika na unayoyasema? Nikienda chumbani mwako sintamkuta mgeni yeyote?"Helen akajibu; "twende chumbani ukajioneee mwenyewe"
Steven hakutaka kunywa chai tena, akamshika mkono dada yake na kwenda moja kwa moja hadi chumbani kwa dada yake. Walipofika chumbani kwa Helena, hakuamini macho yake. Hakukuta msichana yeyote wala dalili za ugeni wowote ndani ya chumba cha dada yake. Nguvu zilimwishia. Akajiuliza; Mungu wangu nimelala na nani jana usiku? Akiwa bado ameduwaa; hajui nini afanye. Akasikia mlio wa meseji ya simu.
Aliposoma meseji alishtuka zaidi; kupata ujumbe kupitia namba +66-666-666.
ITAENDELEA ALHAMIS IJAYO...."Tafadhali itunze siri yetu".Steve, alishtuka kwa uoga. Miguu yake ikaishiwa nguvu. Akaanza kutetemeka kwa uoga. Mungu hii ni namba gani? Jana nimelala na nani? Helena akauliza; "Kaka Steve..una tatizo gani?".Akiwa bado ana kigugumizi; akasikia sauti ya mama yao anaita; "Helena...Helena..mnafanya nini huko na kaka yako? Kuna tatizo gani limetokea?".
TSL-Books
Geophrey Tenganamba
No comments:
Post a Comment